LETSHEGO TANZANIA YABORESHA MIUNDOMBINU YA MAJI KATIKA MAKAZI YA WAZEE NUNGE.
Katika
kuadhimisha miaka 18 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
jumuiya ya wafanyakazi wa taasisi ya fedha ya Letshego Tanzania waliadhimisha
siku hiyo kwa kutembelea makazi ya wazee wasiojiweza na walemavu Nunge, Kigamboni ambapo walipata
nafasi ya kusikiliza mahitaji ya wazee hao na katika jitihada za kutatua baadhi
ya changamoto za wakazi wa Nunge kwa siku hiyo walitoa msaada wa tenki moja la
maji la ujazo wa lita 7000 ikiwa ni pamoja na kulipia gharama zote za ufungwaji
na uunganishaji wa mabomba katika tenki hilo na pia walikabidhi risiti ya
malipo ya umeme luku kiasi cha cha shillingi 500,000 kwa Mkuu wa Kituo cha
Nunge Bwana. Ojuku Mgedzi.
Aidha
Mkurugenzi wa Letshego Tanzania Bw. Yohane Kaduma
ameahidi kutoa pampu kubwa ya maji kwa kituo cha Nunge ambayo itasaidia kulimaliza kabisa tatizo la usambazaji wa maji
katika kambi hiyo.
Mkurugenzi wa Letshego Tanzania, Bw. Yohane Kaduma
(Kushoto) akimkabidhi tenki la maji Mkuu wa Kituo cha Nunge Bw. Ojuku Mgedzi walipotembelea makazi hayo
kusiikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa Tenki la maji, Luku na Mavazi
kwa wakazi wa kambi hiyo juzi.)
Post a Comment