advert banner

advert banner
Advert banner

Unawezaje kufanya kazi kwa ari ileile kipindi cha sikukuu?


Na Jumia Travel Tanzania

Huenda hili jambo la kawaida miongoni mwa watu wengi kuona ugumu kufanya kazi kwa umakini na ari ileile katika kipindi kama hiki cha kuelekea sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.

Hali hii huwa inawatokea wafanyakazi wengi  katika sekta za serikali na kampuni binafsi ambapo shughuli nyingi husimama kutokana na mapumziko ya mwisho wa mwaka; ambayo wafanyakazi wengi hupewa ili kujipanga kwa mwaka mpya ujao.

Kama hali hii huwa inakutokea mara kwa mara na haukuwahi kung’amua ni kwa namna gani utaweza kukabiliana nayo basi Jumia Travel ingependa kukushirikisha mambo yafuatayo iwapo utayafuata kwa ukamilifu basi utakuwa umepata ufumbuzi wake.

Chukua likizo
Taasisi zote huwa zinatoa muda wa mapumziko kwa wafanyakazi wao ili kuwapa muda wa kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zao. Kipindi hiki ni kizuri kuomba likizo kama ulikuwa na muda umebakia. Hii itakuwezesha kuja na ari na umakini mkubwa wa kutekeleza majukumu yako. Kusafiri na kutalii sehemu mbalimbali nchini kunaweza kuwa kitu kizuri sana kwako, jaribu kutembelea mtandao wa Jumia Travel (www.travel.jumia.comna kujionea ofa kamambe kwenye msimu huu wa sikukuu.

Panga na pambanua ratiba na matarajio yako mapema
Ni vizuri kuainisha mapema ni mambo gani ambayo utahakikisha unayafanya kabla ya kipindi cha sikukuu kufika. Ukifanya hivi itakuwa ni vizuri zaidi kwani itakuwezesha kuweka nguvu na umakini mkubwa katika kuyakamilisha. Kila mtu anafahamu pilikapilika za kipindi cha sikukuu kama vile kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali, kusafiri pamoja na kutumia muda mwingi na familia au wapendwa wako.

Usipeleke kazi za ofisini nyumbani kwako
Kuna watu wana mazoea ya kwenda kufanyia viporo vya kazi za ofisini nyumbani kwao. Nakushauri ndani ya kipindi hiki ambacho ari na umakini hupotea kwa haraka sana kuhakikisha unamaliza kila kitu ukiwa ofisini au kukifanya kuwa kipaumbele cha siku inayofautia. Muda wa nyumbani ni vema ukatumiwa kwa mambo mengine kama vile kushiriki shughuli za nyumbani pamoja na familia yako kwani wanahitaji muda huo kuwa nawe.

Epuka kufanya kazi nyingi kwa mpigo
Kama wewe ni bingwa wa kufanya kazi nyingi kwa mpigo kama vile za ofisini na binafsi kwa pamoja nakushauri uache mara moja kwani zitakuondolea umakini na mwishowe kuharibu kabisa. Tenga muda wa kufanya kazi za ofisini ukiwa kazini na binafsi pale unapokuwa na muda wa ziada au baada ya kukamilisha majukumu yako.


Hakikisha unakuwa kwenye ari ya kazi muda wote
Katika kipindi hiki cha sikukuu ambapo mabosi wengi ofisini wako likizo ni vigumu sana akili kutulia na kujikita kwenye kazi. Unaweza kurudisha ari yako na kufanya kazi zako kwa umakini kama siku za kawaida kwani sio siku zote ni sikukuu. Ukilitambua hilo na kujua dhumuni la wewe kuwa kazini basi utakuwa makini.

Fanya mazoezi
Njia mojawapo bora kabisa katika kuhakikisha kuwa unabakia kwenye ari ya kufanya kazi ni kufanya mazoezi na kuzingatia chakula bora. Mazoezi ni dawa nzuri kwa kutibu msongo wa mawazo na kurudisha mwili katika hali yake ya kawaida na kuwa na ufanisi.

Jifanyie tathmini, jipange vema kwa mwaka mpya ujao
Inapofikia mwisho wa mwaka ni vema kujifanyia tathimini sisi wenyewe kwa kuangazia mambo tuliyoyakamilisha ndani ya kipindi chote cha mwaka. Unaweza ukajitathimini kuanzia ngazi ya kazi, binafsi au familia kwa ujumla endapo umefanikisha yale malengo uliyojiwekea wakati mwaka unaanza.

Jumia Travel inaamini kuwa kwa baadhi ya hayo mambo endapo ukiyafuatilia kwa umakini, basi utakuwa na muda mzuri wa kufanya kazi zako ndani ya kipindi hiki cha sikukuu na pia kuwa na mapumziko yenye mafanikio.

No comments

Powered by Blogger.